Jambo La Kustaajabisha

Written by Oluoch Madiang’

(See: http://madiang.wordpress.com/2011/08/12/jambo-la-kustaajabisha/)

Kule Nairobi
Jambo la kustaajabisha lilitendeka-
Jambo la kistaarabu.

Aliingia kwenye karadinga muungwana mmoja wa mjini
Amejibana kwa suti aipapase uchi wake;
Amejinyonga kwa tai aisitiri shingo lake;
Amejifunga pingu kwa saa asipoteze muda wake;
Amejihami kwa kitambara ahifadhi makamasiye.

Aliingia kwenye karadinga muungwana mmoja wa mjini
Akasimama imara muungwana;
Akatabasamu kwa ustahivu muungwana;
Akasubiri kwa utulivu muungwana;
Huku amekamata kwa himaya mfuko wa ngozi (alimotia werevu wake wote).

Aliingia kwenye karadinga muungwana mmoja wa mjini
Mara hiyo hiyo, baradhuli kushoto mwake akavuta kikohozi na kuitema miguuni pake;
Kwa ustaarabu, muungwana hakutingishika wala kubabaika.
Kufumba na kufumbua, mlala hoi kulia mwake akashuta mashuzi ya kukera mno;
Kwa ustaarabu, muungwana akatulia bila hata kuinua pua juu.

Kwa ustaarabu wa kuhusudiwa, muungwana hakumkemea kamwe baradhuli yule –
Kwani huwezi jua alikolelewa huyo baradhuli;
Au alilelewa na pumbavu yupi huyo baradhuli;
Au lini alipata tajiriba ya ushenzi huyo baradhuli.

Kwa ustaarabu wa kuhusudiwa, muungwana hakuinua pua dhidi ya mshutaji yule –
Kwani huwezi jua alikula nini huyo mnyambaji;
Au aliikulia wapi mnyambo huo huyo mnyambaji;
Au kujua, kwa hakika, alinyambwa lini huyo mnyambaji.

Kule Nairobi
Mambo ya kustaajabisha yanatendeka-
Mambo ya ustaarabu!

© OLUOCH-MADIANG’.

Advertisements

Author: Faith Oneya

Lover of the written and spoken word.

Tell me what you think...

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s