Shairi:Kosa Langu…….

Na Gloria Mwaniga

 

Nilipokuona,

moyo wangu  ulipona,

nikajua bila shaka,

wewe ni wangu

Nikakupenda tangu

Na hilo ndilo kosa langu

Ulipoona hivyo

Ukajawa na madaha

Na kuniona mi ovyo

Ukanitupa bila msamaha

Na kufanya nikose raha

Basi nikajifunza kwa kasi,

Uzuri wa mti ndani mkakasi

Nikaacha wasiwasi,

mapenzi yako nikawacha yapasi

Sasa nimetupa biwi la simanzi

Nikampata mwingine manzi,

Jina lake  Lazizi,

anachunga langu zizi,

nami  napata usingizi,

Nimepata  pia kujikosoa,

kuwa  tabia zako za madoa,

Ni zako mwenyewe na wala,

Sio  kosa langu

Advertisements

Author: Gloria Mwaniga Minage

Phenomenal woman. that's me

One thought on “Shairi:Kosa Langu…….”

  1. La haula…hili ni lile ambalo nitalitaja kwa kimombo cha kurembesha kuwa ‘absofabulous’. Shairi nzuri dada…hata nikatamani langu zizi pia lipate kushuhudiwa kwa namba la malenga huyu! 😉

Tell me what you think...

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s